212 NILISIKIA SAUTI YA YESU

1. Nilisikia sauti ya Yesu, Naye aliniambia, "Ufike
Nami nikusaidie Ufike, nakungojea!"


Njoo kwa Yesu ufike upesi, Upokee wokovu wa
Mungu! Mbona kukawa dhambini tena? Yesu
anakuita. Njoo!


2. Ukiwa na hofu kumjia Yesu, Kwa kuwa u mwenye
Dhambi, Kumbuka Yesu ni mwenye huruma. Uje,
Yeye akungoja!


3. Ukiwa maskini, tena dhaifu, Yesu anakufahamu.
Anakuambia, “Pokea neema, Acha mzigo wa
Dhambi!”


4. Na mimi pia nilimfikia Yesu anayenipenda.
Nilipokea wokovu na raha Kwa shangwe
Namshukuru.


Comments