1. Kama unataka kuwa mtu wa Yesu, Na kumfuata
Yeye daima, Kama wataka yeye akusaidie, Umpe
Moyo wako!
Ataondoa dhambi zako zote Na utazipokea nguvu
zake! Ukijazwa Roho utaona Ni vizuri kum-fuata
Yesu
2. Kama unataka kuwa mtu wa heri, Fungua moyo,
Yesu aingie! Kama unataka utulivu na raha, Umpe
Moyo wako!
3. Na ukitaka kumtumikia Yesu, Na kuifuata njia
Yake kuu, Kama unataka kuingia mbinguni, Umpe
Moyo wako!
Comments
Post a Comment