1. Unayekosa amani, Uishiye dhambini, Uje kwa
Yesu Mwokozi! Yeye ukimwamini, Atakuosha
Moyoni Na kukujaza amani, Upate amani, amani
Ya Yesu.
2. Yesu anapokiweka Kiti chake cha enzi Moyoni
Mwako na kukaa, Mapenzi yake Mungu
Yatimizwa hata kwako, Ukimsujudia Bwana.
Upate amani, amani ya Yesu.
3. Amani hiyo ni ngome Ya kutulinda vema,
Yasiingie mabaya Kumhuzunisha Roho. Amani ya
Mungu wetu Ikae nyumbani mwetu.
4. Mlango huko mbinguni Uwazi hata leo Kwa watu
Waaminio Wapate kuingia. Bwana wetu wa amani,
Enyi watu msifuni! Mpate amani, amani ya Yesu.
Comments
Post a Comment