1. Mwenyezi Mungu anafanya Miujiza duniani.
Anaondoa minyororo Ya watu waliofungwa.
Avunja nyavu za Mwovu, Aokoa wakosaji.
2. Maneno yake yana nguvu Kushinda yote ya giza.
Na watu wanapiga mbio, Kuomba neema Ya
Mungu. Wakiisha kusamehewa, Waimba: “Sifa
kwa Yesu!” Tupate amani; amani ya Mungu.
3. Tazama, ndugu wengi sana Wamfuata Yesu Leo.
Katika kila nchi sasa Maelfu wampenda Mungu.
Wengine wengi wavutwa, Kwa Mwenyezi
Mungu Baba.
4. Inua macho, mvunaji, Mavuno sasa yaiva. Uende
kutafuta watu, Uwapeleke kwa Yesu! Ndugu
wote, amkeni, Okoeni wenye dhambi!
5. Najua siku ni karibu Yesu atakaporudi,
Awachukue watu wake Hadi nchi ya amani. Siku
ile ya uheri Natamani kuiona.
6. Wengine watakapofika Kwako mbinguni,
Mwokozi, Nisibakie huku chini, Neema hiyo
Naomba! ’Nichukue mikononi, Unifikishe
Mbinguni!
Comments
Post a Comment