1. Ingaliko nafasi mbinguni, Arusini huko kwake
Mungu. Uje leo! Nawe akuita!
Jioni inakukaribia, Jua lachwa, maisha yapita.
Uje leo! Nawe akuita!
2. Na karamu yake ni tayari, Bwana anakualika
wewe. Uje leo! Nawe akuita!
3. Watu wengi waingia huko. Fanya hima nawe
uingie! Uje leo nawe akuita!
4. Tazama lango lafunguliwa! Neema gani,
kukaribishwa! Uje leo! Nawe akuita!
5. Uje mbio, utaona heri, Yesu akupe neema
nyingi! Uje leo! Nawe akuita!
6. Utaona shangwe ya mbinguni.Bwana arusi
akungojea. Uje leo! Nawe akuita!
7. Unayesitasita waitwa, Amua kuitikia mwito!
Uje leo! Nawe uingie!
8. Ukisita utabaki nje, Na utasikia neno hili:
"Ondokeni! Siwajui ninyi!"
Comments
Post a Comment