217 BWANA YESU ATAKUJA

1. Bwana Yesu atakuja Kutoka mbinguni.
Atawachukua wote Wamwaminio.


Kama nyota za mbinguni Watang'aa milele
Katika taji yake Yesu Mwokozi.


2. Atawakusanya wote wanaompenda.
Watakuwa tunu yake Milele kwake.


3. Na watoto watakuwa Pamoja na Yesu.
Watang'aa kama lulu Kwa Baba Mungu.


Comments