- Yesu u rafiki yangu, Una uwezo kweli,
Wa kuziondoa dhambi, Na kutakasa roho.
Ninaomba masamaha, Nipe ushindi wako,
Unilinde hata mwisho, Unitwae kwako juu. - Mimi nilikuwa mwovu, Sikukupenda Yesu
Kwa hakika sikujua, Wewe na pendo lako. - Bwana Yesu usamehe, Dhambi nilizofanya
Nisishindwe na jaribu, ’nijaze nguvu zako! - Tangu sasa wewe Yesu, U Mkombozi wangu,
Niwe mbali na Shetani, Niwe wako daima!
Comments
Post a Comment