223 NI UHERI KATIKA KUMWAMINI

1. Ni uheri katika kumwamini Yesu Wakati
Wa ujana wetu, Kabla hatujaonja dhambi
Na mashaka Zinazoharibu rohoni.


Ni uheri katika kumwamini Yesu
Na kumfuata daima. Na ujana wetu
Unapotukimbia, Shangwe ya wokovu yabaki.



2. Ni uheri katika kum-tii Yesu Wakati wa
Ujana Wetu. Tutakuwa na dhamiri safi
Na njema Kwa Maisha yetu daima.


3. Ni uheri kumtumikia Mwokozi Wakati
Wa ujana wetu. Yesu anakumbuka kila
Tendo dogo. Atatulipa kwa neema.


4. Ni uheri kumngojea Bwana Yesu Wakati
Wa ujana wetu. Atatuchukua kwake kwa
Furaha kuu, Tutakuwa naye milele.

Comments