225 CHAGUA YESU

1. Chagua Yesu wewe uliye kijana, Umpe Yeye
Moyo wako kwa pendo! Yesu Rafiki
Anayekupenda sana Siku za furaha hata za huzuni.


Chagua Yesu kwa siku zote! Yeye rafiki
wa ajabu. Ukiwa naye katika ujana wako
Hatakuacha tena hata milele.


2. Ni vema sana kuwa naye safarini Anayekufahamu
Katika yote. Hata ukiudhiwa hapa duniani,
Kumbuka Yesu yupo pamoja nawe!


3. Na mwishoni ikiwa umestahimili, Utaipokea
Taji ya uzima. Furaha gani utakapomwona
Yesu Katika utukufu kwake mbinguni!


Comments