1. Ee Bwana Yesu nakushukuru, Ninayo
Haki kuwa wako tu. Katika giza, katika
Nuru Ninayo yote - wewe wangu tu.
2. Wakiniacha rafiki zangu, Ninayo haki
Kuwa wako Tu. Wakidharau uheri wangu,
Si kitu kwangu - wewe wangu tu.
4. Katika shida za hii dunia, Ninayo
Haki kuwa wako tu. Na nikichoka katika
Njia, Si kitu kwangu - wewe wangu tu.
5. Wakinipenda na kunisifu, Ninayo haki
Kuwa wako tu. Wakinitenda uharibifu,
Si kitu kwangu - wewe wangu tu.
6. Ikiwa nina dhahabu nyingi, Ninayo haki
Kuwa wako tu. Ikiwa nina taabu nyingi,
Si kitu kwangu - wewe wangu tu.
7. Kuwa wako tu. Ee, Bwana Yesu,
Watukubali, Mimi ni wako - wewe wangu tu.
Comments
Post a Comment