227 MUNGU BABA MBINGUNI

1. Mungu Baba mbinguni, Alimtuma
Mwokozi, Naye ndiye rafiki ya watoto.
Jina lake ni Yesu, Ni Mwana wake
Mungu, Atupenda sote, wewe na mimi.


Mbingu na ufalme wake Ni kwa watoto
wote. Sasa tushike njia Iendayo kwa
Yesu, Tuione furaha ya mbinguni.


2. Yesu mwenye upendo Aliwakumbatia,
Na kwa huruma aliwabariki. Duniani hayupo
Rafiki kama Yesu, Hawezi kumsahau ye yote.


3. Yesu, Mchunga mwema Awakusanya sasa
Mikononi mwake wana wa kondoo. Na kifuani
mwake, Awatunza daima, Hata kwa ufalme wake
mbinguni.

Comments