1. Ju-u ya mlima uliwekwa mti,
Uliodharauliwa. Msalaba huo
Naupenda sana, Hapo Yesu 'katufilia
Naupenda msalaba huu,
Nitashinda kwa nguvu zake.
Naupenda msalaba huu,
Taji nitapewa huko juu.
2. Msalaba huo naupenda sana, Wengine
Waudharau, Kwani Mwana-Kondoo
Aliacha mbingu, Kutufilia msalabani.
3. Naona uzuri wa msalaba huu, Damu
Ilipomwagika. Hapo Bwana Yesu alisulibiwa,
Mkombozi wa wenye dhambi.
4. Nitanyenyekea penye msalaba, Kuyavumilia
Yote. Nitakaribishwa na Yesu mbinguni,
Kwenye utukufu milele.
Comments
Post a Comment