1. Golgotha Mwokozi aliwambwa,
Akafa kwa 'jili yetu. Yesu akatoa
Damu yake, Ili tukombolewe.
Penye msalaba nilisafishwa Kwa
damu ya Yesu niliokolewa. Mwamuzi
mwenyewe ni Mwokozi, Aliyenifilia.
2. Na nimesulibiwa Golgotha Pamoja
Na Bwana Yesu. Njia ni wazi kwenda
Mbinguni Na pazia halipo.
3. Nimesulibiwa pamoja naye, Na utu
wa kale ulikufa hapo. Mambo ya zamani
yamekwisha, Sasa yote ni mapya!
4. Niliunganishwa na Mwokozi, Sasa ni
Hai kwa Mungu. Kuishi ni Kristo,
Siri kubwa, Na kufa ni faida!
5. Nimetakasika kwa damu yake, hatia
na dhambi zimeondolewa. Shetani
hawezi kunidhuru, Nimepewa uhuru.
Comments
Post a Comment