1. Nilipofika kwa Mwokozi, Nikapaza sauti yangu
“Yesu Bwana, unirehemu! Uniokoe!”
Sifa kwa Yesu, Mwokozi wangu!
Alisikia ombi langu, Sifa kwa Yesu!
2. Nilipofika msalabani, Nikamsihi Bwana Yesu:
“Unitakase, niwe safi.” Akasikia!
3. Chemchemi ya msalabani Hata leo yabubujika,
Kuokoa na kusafisha Wakati wote.
4. Njoo kwa Yesu hata wewe, Unywe, uoshwe moyo
wako: Kiu ipoe, utakaswe, Umsifu Yesu!
Comments
Post a Comment