233 TAZAMA MWOKOZI

1. azama Mwokozi aliyekufilia, Ili nawe
Upate uzima! Tazama kwa pendo
Atakusaidia, Usidumu dhambini tena!


Nawe tazama! Mtazame Yesu
aliyekufilia, Uwe na uzima milele!


2. Mwokozi alisulibiwa juu ya mti, Ili
Sisi tupate wokovu. Alitukomboa kwa
Damu yake safi, Kwake tunapata uzima.


3. Hakuna majuto yaweza kutuponya,
Ila damu ya Yesu Masihi. Ufike kwa Yesu
Upate kuokoka Na kuondolewa hatia.


4. Rafiki, waitwa na Mungu kwa wokovu,
Anataka Ufike upesi. Kwa nini kukawia?
Fika bila hofu, Ondoka katika hatari!


5. Uje, upokee uzima wa milele, Bwana
Yesu Ali’tuletea! Karama ya Mungu ni
Tumaini letu, Ipokee, usipotee!

Comments