1. Utukufu mbinguni Ni wa heri, amani,
Dhambi Haziingii. Vilivyomo mbinguni
Vyote ni vya Thamani, Dhambi haziingii.
Dhambi haziingii Mbingu yo. utukufu. Ukidumu
Dhambini pasipo kutakaswa, Huingii mbinguni.
2. Ukiwa na kusudi kuingia mbinguni,
Kumwona Bwana Yesu, tafuta utakaso,
Uwe safi moyoni! Dhambi haziingii.
3. Unapotenda dhambi,Wamkana Mwokozi,
Kumbuka,ndugu yangu; Dhambi Zitalifunga
Lango la utukufu.Dhambi haziingii.
4. Ukiwa mkaidi Hata saa ya kufa, Utatoa
Hesabu. Tena utaambiwa; ”Ondoka
Sikujui! ”Dhambi haziingii.
5. Ukitaka kufika mbinguni kwenye raha,
Tubu, uache dhambi, Mpokee Mwokozi,
Nawe utaingia!
Comments
Post a Comment