1. Tumeokoka toka dhambi, Usikilize, ee rafiki!
:/:Tumeokoka tufike juu, Kuvikwa taji. Furaha
kuu!:/:
2. Tumeokoka, tu salama, Wakitucheka - ni kwa
muda! :/:Twavumilia shida zote Twatazamia heri
kule!:/:
3. Tumeokoka, tuko huru, Tukichokozwa haidhuru.
:/:Tutaiacha dunia hii Na kukaribishwa
mbinguni!:/:
4. Tumeokoka. Furaha kuu! Twaandaliwa karamu
Juu! :/:Salamu hiyo utangaze, hata wengine
Waokoke!:/:
5. Kwani kungoja Mama, Baba? Twende pamoja
Ndugu, Dada! :/:Hataingia asitaye. Yesu akwita:
Leo uje!:/:
Comments
Post a Comment