237 JINA LA YESU NDILO MWAMBA

1. Jina la Yesu ndilo mwamba, Ahadi zake imara,
Zinaniletea amani Na mibaraka daima. Katika
mwamba ni raha kuu, Baraka tele kutoka juu.
Nakaa humo, nastarehe, Ni maisha ya uheri.


2. Na mwamba huu ni kimbilio Katika hali yo yote;
Adui nisimkimbie, Nishinde katika yote. Dunia
ikitetemeka, Ahadi zake zasimama. Nakaa humo,
nastarehe, Ni maisha ya uheri.


3. Naishi mbali na hatia, Udhalimu na hukumu.
Nikisimama kwa imani, Adui atakimbia. Naacha
mawazo ya giza, Nafasi hayataipata. Nakaa
humo, nastarehe, Ni maisha ya uheri.


4. Ninafurahia baraka Za ulimwengu wa roho.
Karama hizo nilipewa Katika kufa kwa Yesu. Sioni
woga na mashaka, Manung'uniko wala shida.
Nakaa humo, nastarehe, Ni maisha ya uheri.

Comments