1. Nifananishwe nawe Mwokozi,
Ni ombi langu liillo kuu. Ninakuomba
na kwa machozi, Nikufuate, Bwana Yesu!
Nifananishwe nawe Mwokozi, Mwenye upendo, safi
kweli! Unitakase, Unijalize, Nifananishwe nawe Yesu!
2. Nifananishwe nawe Mwokozi,
Mwenye rehema na upendo! Niwapeleke kwa
Mkombozi Walioshindwa majaribu!
3. Nifananishwe nawe Bwanangu,
Mwenye saburi, Mtakatifu! Niwe mnyofu kazini
mwangu, Mtu thabiti na wa kweli.
4. Nifananishwe nawe Mwokozi!
Nakuomba: Unijalize! Vyote ninavyo nakutolea,
Uniongoze siku zote!
5. Nifananishwe nawe Mwokozi!
Nimiminie pendo lako! Unitakase kwa damu yako,
Nistahili kwako mbinguni!
Comments
Post a Comment