1. Mungu Baba aliye mbinguni Amenifurahisha
Moyoni. Ananihakikisha rohoni Yesu yu nami,
Ananipenda.
Anipenda Yesu Mwokozi, Ananipenda kwa kweli.
Anipenda Yesu Mwokozi, Anipenda kweli.
2. Nikipotea toka njiani Bwana Yesu atanitafuta.
Ataniita nirudi kwake, Yesu Mwokozi ananilinda.
3. Nikitazama msalaba wake Na jinsi alivyojitolea,
Ninampenda Mwokozi wangu Aliyenifilia
Golgotha.
4. Kumfahamu yanipa raha Na kumwamini kuna
furaha. Amekwisha shindwa yule mwovu, Nina
ushindi katika Yesu.
5. Sifa ni nyingi kwake Mwokozi Nami nitamsifu
daima. Hata mbinguni nitamwimbia MwanaKondoo, Yesu mpendwa.
Comments
Post a Comment