1. Ninaufurahia uzuri wake Yesu Unaopita fahari yote ya dunia, mawazo yangu hayawezi kuufahamu. Uzuri wake wazidi kuwa bora kwangu.
Nashindwa kueleza uzuri wa Yesu, Ila nitaufahamu kamili mbinguni.
2. Upendo wa ajabu ninausifu sana, Ukanivuta kwa upole nije kwa Bwana, Ukaniondoa katika unyonge wangu, Upendo wake wazidi kuwa bora kwangu.
3. Nashindwa kueleza wokovu wa Yesu, Ila nitaufahamu kamili mbinguni.
4. Ninausifu wokovu wake wa ajabu, Uliondoa woga, wanipa utulivu. Nampenda Yesu aliyechukua dhambi, Wokovu wake wazidi kuwa bora kwangu.
5. Nashindwa kueleza upendo wa Yesu, Ila nitaufahamu kamili mbinguni.
Comments
Post a Comment