1. Kumtegemea Mwokozi kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake Nina raha moyoni.
Yesu, Yesu namwamini, Nimemwona thabiti.
Yesu, Yesu yu thamani, Ahadi zake kweli.
2. Kumtegemea Mwokozi Kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake Nimeoshwa kamili.
3. Kumtegemea Mwokozi kwangu tamu kabisa.
Kwake daima napata Uzima na amani
4. Nafurahi kwa sababu Nimekutegemea.
Yesu, Mpendwa na rafiki uwe nami daima.
Comments
Post a Comment