1. Wasafiri mwaendapi, Mwaenda nchi gani? Sisi
Kweli Ni hakika Tumeanza safari. :/:Tumesikia ya
Kwamba Kuna nchi ya mbinguni. Tumeitwa naye
Mungu Ndiko tunakokwenda.:/:
2. Kuna mambo gani huko? Mtueleze nasi! Twaenda
Kwa Bwana Yesu Kwenye makao mema.
:/:Tutamwona uso wake Na kupendana kindugu.
Tutakaa naye Yesu Milele na milele:/:
3. Wasafiri tujiunge, Tusafiri pamoja! Jitayarisheni
Sasa Kupatana na Mungu. :/:Yesu ni Mwokozi
Kweli kwa wote wamwaminio. Mnaomwamini
Njoni, Twende sote mbinguni!:/:
Comments
Post a Comment