245 MIKWAJU ITIAPO GIZA

1. Mikwaju itiapo giza na kivuli katika nchi ya
Bersheba zamani, Alitembea Ibrahimu asubuhi
Akiwa mwenye maumivu rohoni kwa kuwa
Aliitwa na Mwenyezi Mungu Kutii amri yake bila
Kusita, Na hapo akaomboleza: "Ee Bwanangu,
Wataka nikutolee mwana wangu?"


2. Alipoamka Ibrahimu alfajiri, akatandika punda,
Kuni 'kazitwaa. Akasafiri pamoja na mwana wake.
Roho yake ikalia kwa huzuni. Mwanawe Isaka
Aliyemfurahia, Kipeo cha furaha ya uzee wake,
Matumaini yake yote ya dunia, Kafara atakayotoa
Kwa Bwana.


3. Katika njia ya mlima wa Moriya Mtoto akamsaili
Babake "Tazama moto uko, kuni ziko pia, Kondoo
Mume kwa kafara yuko wapi?" Na Ibrahimu
Akamjibu kwa imani Isiyokuwa na mashaka yo
Yote: "Kondoo mume kwa kafara ya shukrani
Naamini Mungu atajipatia."


4. Je, awezaje Ibrahimu kusahau Siku hiyo ya
Uchungu na huzuni, Na jinsi akajenga huko
Madhabahu Na kumweka mwana juu ya kuni?
Akakitwaa kisu amchinje mwana, Halafu alisikia
Neno tamu: "Usimnyoshee kijana mkono wako,
Ninajua kwamba unamcha Mungu!"


5. Akainua macho yake kwa haraka Akaona
Kondoo mume nyuma yake, Aliyenaswa pembe
Zake kichakani! Akamtwaa badala ya mwanawe.
Na malaika akamwita, akanena: "Umenisadiki,
Nitakubariki. Na kwa uzao wako mataifa yote
Watabarikiwa Kwani umenitii."


6. Tangu hapo machozi yamekuwa mengi Na watu
Wa Mungu wamejaribiwa Wakimtolea Mungu
Dhabihu zao Na kwa njia hiyo wamekamilika. Hata
Leo juu ya mlima wa kafara Mungu anawabariki
Watu wake. Awajulisha nguvu zake na ishara,
Awajaliza Roho na moto wake.

Comments