247 NAPENDA SANA KUMSHUKURU

1. Napenda sana kumshukuru Mwokozi Wangu kwa nia huru. Kwa wimbo wangu Nashuhudu juu ya pendo lake na damu.


2. Ninapoona mateso yake Msalabani na Kifo chake, Hapo nataka kumwimbia Wimbo wa shukrani na sifa.


3. Naimba sana, nina faraja, Katika Yesu Nina taraja. Maneno atufunulia, Kwa Wenye dhambi yamefichwa.


4. Kwa neno lake aniambia Ya kwamba Ananihurumia. Sasa ninao ukombozi, Ninatakasika damuni.


5. Na msione ajabu sana Kwa kuwa Namshukuru Bwana. Huku naanza Kumwimbia, Mbinguni nitaendelea.


6. Anipa vyote kwa pendo lake, Urithi Wangu wachungwa kwake. Nitashangilia Wakati Ninapoingia mbinguni.

Comments