249 ZAMANI WAISRAELI

1. Zamani Waisraeli walisali Mjini Yerusalemu.
Wakristo wa sasa wanakusanyika Kumwabudu
Bwana Yesu.


Msifuni, msifuni, Mungu wetu Kwani
atutendea mema! Tutamsifu tu, aliyetoka
juu. Mshangilieni Mwokozi mwema!


2. Mwokozi yu nasi anadhihirisha. Uwezo wa kuokoa.
Na yu mwaminifu, atusikiliza, Apenda kutubariki.



3. Twaomba baraka na mvua ya mbingu.
Alithibitishe Neno! Wagonjwa wapone, vipofu
waone, Tujazwe Roho wa Mungu

Comments