25 MVUA YA MBINGU UNYESHE

  1. Mvua ya mbingu unyeshe, Juu ya dunia yote, Kama ulivyoahidi; Tunaingoja Bwana.


    Mvua ya mbingu, Roho Mtakatifu! Utunyeshee baraka, Tunakuomba Mungu.


  2. Mvua ya mbingu unyeshe, Tuam-shwe na sisi! Mabondeni milimani, Mvua itufikie!


  3. Mvua ya mbingu unyeshe, Ulimwenguni mwote! Watu wapate kupona, Neno lako lienee!


  4. Mvua ya mbingu unyeshe, Tunakuelekea! Utujalie baraka, Ee Mungu tunaomba!

Comments