1. Nilipomwamini Yesu Ikawa kwangu
siku kuu. Rohoni mwangu namsifu.
Yesu yu Mwokozi wangu.
Siku kuu, siku kuu! Yesu aliniokoa!
Kwa neema na upendo akanisamehe
dhambi. Siku kuu, siku kuu! Yesu ameniokoa
2. Nafurahi kuokoka Na kuitwa mwana wake. Alinivuta kwa pendo Nami nikamfuata.
3. Nashangilia moyoni Nikimfuata Yesu.
Neema yake yatosha Katika maisha yangu.
4. Kwa pendo kuu na rehema Ananitunza daima.
Sisahau siku ile Nilipomwamini Yesu.
Comments
Post a Comment