1. Yesu, Mwamba wa kale, Kwako ninajificha.
Maji yale na damu, Kutoka ubavuni,
Yaweza kuniponya Mwili, Nafsi na roho!
2. Kazi za wanadamu, Hazileti wokovu.
Ningekuwa na bidii Na kulia machozi,
Dhambi bado ziko tu, Uniokoe Yesu!
3. Kweli mimi si kitu, Mimi niko dhaifu.
Ni uchi, naja kwako, ’Nivike utukufu!
Nioshe niwe safi Mbele yako, Mwokozi!
4. Nitakapofikia, Mwisho wa siku zangu,
Nitaitwa na Wewe, Mbele ya uso wako,
Uliye mwamba wangu, Utanificha kwako.
Comments
Post a Comment