1. Siku ya kuisikia parapanda ya Mungu,
Ikiita watakatifu wote, Kwa neema
Tutakaribishwa naye Mwokozi,
Katika kutano kubwa huko juu.
Tutakaribishwa kwake, Tutakaribishwa kwake,
Tutakaribishwa kwake, Katika kutano kubwa
huko juu.
2. Waliokufa katika Kristo watafufuka, Tulio hai
Tutabadilika. Sote tutanyakuliwa kukutana na
Yesu, Tutakusanyika wote huko juu!
3. Mbinguni wimbo utavuma kama maji mengi,
Tutaona utukufu wa Yesu. Na mimi kwa neema
Nitafika siku ile, Nitasikia: “karibu
Mwanangu!”
Comments
Post a Comment