1. Mkutano gani ule Mlimani mwa Sayuni,
Usiohesabika? Ni walionunuliwa, Ndio
Waliotakaswa, Wawe malimbuko kwa Bwana.
2. Walimfuata Yesu, Wakawa waaminifu, Hata
Siku ya kifo. Sasa wanakaa mbinguni,Wametoka
Kwenye dhiki, Wamerithi raha milele.
3. Ukamili wa uzuri, Wa muziki na Zaburi,
Unatoka huko juu. Ni sauti tamu mno Ya kinubi
Na ya wimbo Wakimtukuza Mwokozi.
4. Wimbo gani wanaimba, Sauti kama maji mengi,
Unatia raha kuu? Ndio wimbo mpya ule
Uimbwao sasa kule, Ili kumhimidi Mwokozi.
5. Bwana, unipe ushindi, Unisafishe ulimi, Nami
Niimbe huko! Nipe vazi la arusi, Safi sana, la
Kitani, Lifaalo huko mbinguni!
Comments
Post a Comment