- Nakuhitaji Yesu, Ee Mwokozi wangu,
Sauti yako nzuri, Iniburudishe!
Nakuhitaji Yesu, Mchana na usiku,
Katika sala yangu, unibariki! - Nakuhitaji Yesu, Nionyeshe njia,
Na unitimizie ahadi za neema! - Nakuhitaji Yesu, Unikaribie,
Nipate kuyashinda, Majaribu yote! - Nakuhitaji, Yesu, Kwa mipango yote,
Kwa kuwa bila wewe, Maisha ni bure! - Nakuhitaji, Yesu, Hapa duniani,
Nipate kuwa kwako, Milele mbinguni!
Comments
Post a Comment