260 SASA NIMO SAFARINI

1. Sasa nimo safarini, Naenda mbinguni juu.
Asifiwe Bwana Yesu! Nchi ya uzima wa
Milele, Giza halimo. Asifiwe Mwokozi


Amina, Haleluya! Sasa naenda mbinguni.
Asifiwe Bwana Yesu! Amina, Haleluya!
Sasa naenda mbinguni, Asifiwe Mwokozi.



2. Sasa naenda mbinguni, Penye makao mema.
Asifiwe Bwana Yesu! Yeye amekwenda
Kutuandalia mahali, Asifiwe Mwokozi!


3. Sasa naenda mbinguni, Nchi ya raha nyingi,
Asifiwe BwanaYesu! Watakatifu wa nchi zote
Wataingia, Asifiwe Mwokozi!


4. Sasa naenda mbinguni, Nitamwona Mwokozi.
Asifiwe Bwana Yesu! Nitamsifu kwa neema
Yake ya ukombozi, Asifiwe Mwokozi!

Comments