261 MSAFIRI ULIYE NJIANI

1. Msafiri uliye njiani, Watamani nyumba ya
Baba, Sikiliza nyimbo za mbinguni! U karibu
sana kufika.


Utakuwa huko Pamoja na watakatifu wote,
Mbinguni kwa raha ipitayo fahamu?
Utakuwa huko Wakati wa kuimba wimbo mpya
wa kumsifu Mwokozi milele?


2. Sikiliza sasa makengele, Yapigwayo huko
Mbinguni, Ili kutuita sisi kwake, Mwishoni
Mwa safari yetu.


3. Labda siku ile ni karibu, Nitakapohamia huko,
Sitaona majaribu tena, Nitajazwa na furaha kuu.


4. Lango la mbinguni liko wazi, Mwokozi
Amelifungua, Unawaeza kuokoka kweli,
Usiache uheri wako!

Comments