1. Bado kitambo – vita itakwisha, Kitambo,
Na dhoruba zapoa. Na tena nitalaza
Kichwa changu Mbavuni mwake
Anipendaye. : /:Mbinguni hazitakuwamo
Dhambi, Nitaziona raha na amani.: /:
2. Bado kitambo – roho yaumizwa, kitambo,
Kati’ usiku huku. Machozi ninatoa mara
Nyingi, Maana bado sijamwona Yesu.
: /: Lakini asubuhi ya milele, Huko
Mbinguni sitalia tena.:/:
3. Bado kitambo – cha uchovu huku,
Kitambo na nitamwona Yesu, Na huru
Mbali ya hatari zote, Nastarehe mikononi
Mwake. : /: Uvuli wote utaondolewa, Kwa
Nuru huko kamilifu kweli. :/:
4. Mateso yangu hayadhuru tena,
Nitayasahau kwake Yesu, Nikisumbuka
Hapa duniani, Mbinguni nitastarehe
Kweli. : /: Na Mungu atafuta kila chozi,
Ataondoa maumivu yote. :/:
Comments
Post a Comment