263 ENYI KANISA LA MUNGU

1. Enyi Kanisa la Mungu Punde vumilieni!
Kati’ nchi ya milele, Mtaona amani.
:/: Kitambo kidogo, Na vita itakwisha. :/:


2. Usilogwe na dunia, Usiache wokovu!
Katika shida na raha, Umfutae Yesu tu!
:/: Daima, daima, Utashinda ubaya. :/:


3. Ukichoka safarini, Njia ikiwa ndefu,
Kwa hatari za jangwani, Mungu atakulinda.
:/: Raha ya mbinguni, Yamtuliza msafiri. :/:


4. Kwa imani tunaona, Nchi yetu ya raha,
Ni habari nzuri sana: Majaribu yakoma.
:/: Twendeni, twendeni, Tukutane mbinguni!:/:


5. Tukifariki dunia, Kwa furaha twaenda,
Tulivyovitumaini, Ng’ambo tutaviona.
:/: Furaha, furaha, Furaha ya milele.:/:

Comments