1. Twendeni Wakristo wam-pendao Yesu,
Tumwimbie na furaha , tumwimbie na furaha
Kitini kwa Mungu, kitini kwa Mungu.
Twendeni mbinguni sisi tuliookoka,
Twendeni tukatazame fahari ya Bwana wetu.
2. Hawatafurahi wasiomjua Yesu,
Bali tuokolewao, bali tuokolewao,
Tum-sifu pote, tum-sifu pote.
3. Tuna mibaraka yake, Mwokozi tele,
Kabla hatujafikia, kabla hatujafikia
Mji wake Mungu, mji wake Mungu.
4. Kwa hiyo twendeni furaha izidi,
Tuache huzuni zote, tuache huzuni zote,
Tufike kwa Yesu, tufike kwa Yesu.
Comments
Post a Comment