265 TU WASAFIRI

1. Tu wasafiri, twakaribia Nchi ya Mbingu
kwa Mungu, Tusiogope bonde la kifo,
Yesu anatuongoza.


:/:Tu wasafiri :/: Tutatkutana kwa Baba Mungu,
Ee Bwana Yesu, utuongoze, Tufike sote
mbinguni.


2. Wengi katika wapendwa wetu, Wamevuka
mto wa kifo. Walifuata wito wa Mungu,
Wakahamia huko juu.


3. Katika mwendo wa duniani, walimtazama
Mwokozi.Na waliacha mambo ya huku,
Walimpendeza Yesu.


4. Ndugu wapendwa, tuendelee, Hata
Tukiwa na shida!Yesu ni njia, kweli,
Uzima, Tumfuate daima!

Comments