267 BABA NAKUOMBA

1. Baba, nakuomba asubuhi hii,
Niongoze kweli katika yote.


Ee, Baba sikia Maombi yangu.
Nakusifu Baba, Wanisikia.


2. Ninapoifanya kazi ya leo,
Unitie nguvu, naomba Bwana.


3. Mchana uishapo, usiku waja,
Baba unilinde, ninakuomba.


4. Maadui wengi wananiwinda,
Maishani mwangu. Mungu ’nilinde!


5. Siku zangu zote ulimwenguni,
Niwe na amani, hadi mwishoni.

Comments