1. Ee Yesu ingia rohoni mwangu, Ili nitakaswe
Niwekwe huru, Nipate kushirikiana nawe,
Katika mateso na raha yako.
Nifahamishe uwezo wako! Nisulibishwe
pamoja nawe! Nifahamishe uwezo wako!
Nisulibishwe pamoja nawe!
2. Siombi ufalme, siombi sifa, Naomba neema
Yako daima, Nijue yakini ya msalaba, Ulipokufa
Kwa ajili yangu.
3. Ingia rohoni, unichunguze, Unisaidie katika
Yote, Kusudi nipate nia moyoni, Nijitoe kweli
Kwako Mwokozi.
4. Hakuna neno la kunizuia, Kuwa na umoja
Nawe Mwokozi, Nitawezaje kufika mbinguni,
Nisipounganishwa naye Yesu?
Comments
Post a Comment