269 ENENDENI ULIMWENGUNI

1. Enendeni ulimwenguni, Milimani
Hata mabondeni Kuihubiri Injili,
Msifuni Bwana Yesu!


Msifuni Yesu! Msifuni Yesu! Tangazeni
Neno lake! Msifu Bwana Yesu!


2. Mchana hata na usiku, Eneza Neno la
Bwana Yesu, Nuru inapotokea, Msifu
Bwana Yesu!


3. Na kama vile malaika, Wanavyomhimidi
Mwokozi, Nasi tumwimbie hivyo, Tumsifu
Bwana Yesu!


4. Mwenzangu kabla hujaitwa, Kuondoka
Hapa duniani, Ujisafishe damuni! M-sifuni
Bwana Yesu!

Comments