Skip to main content
- Una uhodari leo, Kumfuata Mwokozi,
Hata ukichekwa sana, Na kupata mateso?
- Una uhodari leo, Kuwa mtu wa Mungu,
Ukiona haya sasa, Mwisho itakuwaje?
- Mji unaonekana Ukiwa mlimani,
Hivyo na imani yetu, Ionekane wazi.
- Ukimpenda Yesu sana Kuliko vitu vyote,
U tayari kum-kiri, Mbele ya watu wote.
- Chuki au pendeleo Yote ni bure kwako,
Watafuta siku zote, Sifa za Yesu Kristo.
- Ujihoji nafsi yako Ukitaka wokovu,
Uliyem-kana Yesu, Utubu dhambi zako!
- Umsihi masamaha, Akuoshe kwa damu,
Omba uhodari sasa, Kumfuata Mwokozi!
- M-chague Yesu leo, M-fuate daima,
Ukitwaa msalaba, Utapokea taji!
Comments
Post a Comment