1. Ninashikwa na kiu, Bwana, unipe maji,
maji ya uhai ndani ya maisha yangu.
:/: Bwana, Bwana, Yesu Mfalme wangu!:/:
2. Moyo wangu wakupenda, Bwana
Mungu wangu. Nitakuja lini kwako,
Bwana Mfalme wangu?
3. Mchana na usiku Bwana nakulilia. Watu
Wanasema: “Mungu wako yuko wapi?”
4. Huzuni moyoni mwangu, Bwana Mungu wangu.
Watu wengi wadharau, Mungu ’wasamehe!
5. Twashikamana pamoja
kwenda juu mbinguni.
Twashukuru, twafurahi kushirikiana.
6. Mwokozi, nguvu zaishaje
moyoni mwangu?
Unisaidie Bwana,
nitakushukuru.
Comments
Post a Comment