1. Ni uheri kumwamini Mungu, Kama Ibrahimu
zamani. Hakutiwa shaka kwa uchungu,
Ila alitii kwa imani. Ni uheri kuendea sawa,
Katika mapito ya kweli. Ukijaribiwa na kukawa,
Mwisho wake utajaliwa.
2. Mashujaa wote wa Biblia, Hawakufuata anasa.
Wakafunzwa kum-tegemea, Mungu Baba
mwenye uweza, Nao wakaenda kwa imani, Ya
kutetemesha dunia Wakashinda giza na Shetani,
Sifa na heshima kwa Mungu.
3. Yeye atakayekuzwa naye Kwanza
atajinyenyekeza. Baba anayempenda mwana
Anamrudi kwa upendo. Hivyo Mungu
anawakamilisha Watu wake wanapoteswa. Na
zaidi kuwafahamisha kulijua pendo lake kuu.
4. Na ikiwa raha ya dunia Yatoweka kwa majaribu.
Mwaminifu atamfurahia Mungu kwani yupo
karibu. Na mavuno ya taabu yake Yakiteketezwa
motoni, Atamtegemea Bwana wake Kwa hiyo
hatanung’unika.
5. Jipe moyo enyi kundi dogo msiogope hatarini.
Shika neno la Mwenyezi Mungu liwaongoze
safarini. Haleluya kwani majaribu yanahimiza
msafiri. Naye ataona kwa karibu Mji wa amani
Mbinguni.
Comments
Post a Comment