1. Ee Mungu mwenye haki, niongoze huku Katika
mambo yote yakupendezayo. Bila Wewe,
Bwana Yesu, mashaka mengi ninayo Ya
kunitisha hapa safarini mwangu.
2. Ee Mungu mwenye haki, niongoze huku Katika
mambo yote yakupendezayo. Bila Wewe,
Bwana Yesu, mashaka mengi ninayo Ya
kunitisha hapa safarini mwangu.
3. Nina safari sasa ya kwenda mbinguni.
Mwokozi yuko huko, Lazima nifike. Na siku ya
kuingia Nitashangilia kweli Kumwona na kumsifu Mwokozi wangu.
4. Ulimwenguni huku kuna shida nyingi.
Nikihitaji kitu, ninahangaika. Lakini siku ile kuu
nitakapomwona Yesu, Natumaini sitaikosa
thawabu.
5. Mbinguni sitaona uovu wowote. Wala kukuta
mambo ya huzuni tena. Sauti nitamtolea
kusema: “Ee, Mungu mwema!” Mikono
nitaipepea kwa shangwe kuu.
Comments
Post a Comment