1. Ee Mungu mwenyezi, matendo yako Yapita
fahamu zote, Lakini hakika najua kwamba Njia
yako ndiyo bora.
2. “Mtoto wangu huwezi kujua Jinsi
nikutendeavyo Lakini usiogope mwanangu,
Mateso yote ’takwisha.”
3. Ee Bwana, unayo magari mengi Na lile
linalonifaa Unichagulie mwenyewe, Bwana,
Nifike salama kwako!
4. Na kama nitaondoka haraka Kama Eliya
zamani, Uchungu na shida zote ’takwisha,
Nitakwenda kwa amani.
5. Tutamsujudia Yesu pamoja Na watakatifu wote.
Mungu mwenye haki hata milele Katika
matendo yake.
6. Nangoja kwa uvumilivu sasa Kuchukuliwa na
wewe. Natarajia uzima milele, Urithi wangu
mbinguni.
Comments
Post a Comment