1. Nitakapotoka duniani, Na kusimama mbele za
Mungu, Nitamwona Mkombozi wangu, Itakuwa
utukufu kweli.
Itakuwa utukufu, utukufu, utukufu
Kumwona Yesu Mwokozi wangu. Itakuwa
utukufu kweli.
2. Huko mbinguni nitakapokaa Pamoja nao
watakatifu, Nitamshukuru Mwokozi wangu,
Itakuwa utukufu kweli.
3. Nitawaona wenzagu wote Waliozishinda
dhambi zote. Na nitamwona Mwokozi wangu,
Itakuwa utukufu kweli.
4. Je, ndugu umejitayarisha Kumwona Yesu
Mwokozi wako, Ili na wewe ushangilie, Na
kuona utukufu kweli?
Comments
Post a Comment