28 NAPENDA NIKUFUATE WEWE

  1. Napenda nikufuate wewe, Yesu daima,
    Nikiwa katika shida, dhiki au furaha,
    Unaponitangulia, Ninakuja nyuma mbio,
    Ninajua ni karibu, Kuwasili kwako juu.


  2. Haifai niulize, Bwana waenda wapi?
    Au kwa kusitasita, Kushika njia yako.
    Kweli hapa kazi moja, Ni kukufuata Bwana,
    Kwenda njia ile moja, Unayonionyesha.


  3. . Ukiona kitu tena, Chataka kunifunga,
    Au kuwa mgogoro, Katika njia yangu,
    Kata kamba mara moja, Ifungayo roho yangu!
    Ninataka kuwa huru, Na kukutumikia.


  4. Bwana Yesu unilinde! Hifadhi nia yangu!
    Nikichoka kwa safari, Nong’oneza kwa pendo:
    “Mwana u mtoto wangu, Uniandamie punde,
    Utapumzika sana, Tena kwangu huko juu!”

Comments