281 YOTE NINAYO NI KWA NEEMA

1. Yote ninayo ni kwa neema, Tangu
Nilipomwamini Bwana, Dhambi na hatia
Zikafutwa, kwa neema yake nimeokoka.


Ameniokoa, Mwokozi Niliyekuwa mwenye
Dhambi, Niliyekufa nimefufuliwa, Kwa
neema yake nimeokoka!


2. Nilitawaliwa na Shetani, Kuelekezwa
Upotevuni, Bali Yesu akanitafuta,
Kwa neema yake nimeokoka.


3. Natakaswa na Yesu Mwokozi, Si kwa
Majuto wala machozi, Bali kwa damu
Nakombolewa, Kwa neema yake nimeokoka


4. Nimejaa shangwe na furaha, Na ninaimba
Nashangilia, Kwa kuwa amenirehemia
Kwa neema yake nimeokoka.

Comments