282 UKIUHITAJI KWELI UTUKUFU

1. Ukiuhitaji kweli utukufu wa Bwana,
Ujalivu wa Roho, Shika Neno la ahadi na
umwendee Baba kwa njia ya imani!


Atajaza moyo wako ufurike. Bwana Yesu
aita, Njoo bila kusita! Atajaza moyo wako
afurike Roho Mtakatifu.


2. Vichukue vyombo vyako, vioshe viwe safi
Kisimani Golgotha. Ujitoe kabisa kwa
Baba na utapewa, Roho moyoni mwako.


3. Mafuta hububujika hayakomi kabisa,
Kadhalika upendo. Anataka kukujaza na
Roho wa ahadi, Mpokee kwa imani!

Comments